Adbox

Thursday, September 26, 2019

Dkt. Zainab asisitiza Matumizi ya Takwimu kwenye huduma za Afya

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt Zainab Chaula, amewataka waganga wakuu wa Mikoa,Wilaya kuhimiza watendaji wa hospitali kujenga Utamaduni wa kutumia takwimu katika huduma wanazotoa ili kuhakikisha usalama wa wagonjwa katika maeneo yao ya kazi.

Dkt Zainabu  ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kongamano la siku tatu lililondaliwa na Chuo kikuu Cha Mzumbe la tathmini ya miradi ya Afya na kufuatilia maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini.

Dkt Zainab amesema lengo la kutaka kutumika kwa takwimu hizo ni pamoja na kutaka kila mmoja katika sekta ya afya aone umuhimu wa kutumia takwimu katika kazi kulingana na kitengo chake.

"Hakuna kitu kizuri kama kutumia takwimu hispitalini au sehemu yoyite ya kazi,kwa sababu itakuwasaidia kutoa majibu mazuri mbele ya jamii," amesema Dkt Zainab Chaula.

Aidha Dkt Zainab amewasisitiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakuu wengine wanaohusika katika sekta ya afya za umma na binafsi kukumbuka kuwapeleka watendaji wao wa ngazi za chini kupata mafunzo ya takwimu ili wajue umuhimu wa kuzitumia.

"Wakuu wote mnatakiwa kujua umuhimu wa takwimu,lakini mkumbuke kwamba huwezi kupata takwimu nzuri kama mtendaji wako wa chini unambana humpi nafasi ya kwenda kuhudhuria mafunzo ya takwimu," amesema.

Amebainisha kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi toka sehemu tofauti lakini ukifuatilia tatizo unalikuta linazunguka hapo hapo kinachotakiwa watendaji wakuu mbadilike kupitia ushiriki wa kongamao hilo.

Kwa upande wake mshiriki wa Kongamano hilo kutoka Chuo Cha Mzumbe, Dkt Eliza Mwakasangula, amesema chuo Cha Mzumbe kwa kushirikiana na chuo kikuu Dodoma (UDOM),Muhimbili,Chuo cha madaktari Ifakara ambavyo vinafanya kazi katika suala zima la utafiti katika matumizi ya takwimu kwenye sekta ya afya.


Dkt Mwakasangula amesema matokeo yanaonyesha kuwa kwenye mitaala matokeo ambayo wanaosoma fani hiyo katika ngazi ya certficate na Diploma kuna msisitizo mdogo kwenye matumizi ya takwimu hivyo ni vema hilo likafanyiwa kazi ili wote kutilia mkazo  suala la utumiaji takwimu.

No comments:

Post a Comment

Adbox