Na Thabit Madai, Zanzibar.
Rais wa Zanzbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Muhamed Shein amesema kuwa Mabunge ya Afrika yanahitaji kupiga hatua zaidi kwa kutumia mfumo wa Tecknologia ya mtandao (e-Parliament,) katika uendeshaji wa shughuli za kibunge kwa lengo la kuchochea Democrasia na maendeleo ya Nchi Zao.
Amesema mfumo huo unaojuikana kwa jina la Bunge Mtandao (e-Parliament) utasaidia kuleta uwajibikaji na kupunguza harama mbali mbali za uendeshaji wa Shughuli za mabunge hayo.
Kauli hiyo ameitoa leo Septembar 2, Wakati akifungua Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya Madola kanda ya Afrika ambapo Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Madinat Al Bahar Mbweni Mjini Magharib Unguja.
Mkutano huo umhudhuriwa na Maspika ,Manaibu Spika na wabunge zaidi ya 400 kutoka katika Nchi ya 19 ya chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika.
Dkt Shein alisema kuwa mfumo huo wa Bunge mtandao (e-Parliament) utakapo tumiwa ipasavyo na mabunge hayo ya Afrika itasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza harama za uendeshaji wa shughuli mbali mbali ikiwemo usafiri za na kuchochea democrasia kwa uwajibikaji kwa wabunge.
Aliongeza kusema kuwa iwapo wabunge na mabunge ya afrika yatatumia mfumo huo itasadia kwa kiasi kikubwa kuleta ukaribu baina ya wabunge na wananchi wao.
“Mfumo huo utakapo tumika utatoa fursa sasa kwa wabunge kuwa karibu zaidi na wananchi wao kwa kupokea maoni na hoja mbali mbali zinazogusa maisha yao kwa urahisi na haraka” alieleza Dkt Shein.
Katika hatua nyingine Dkt Shein alieleza kuwa Technolojia ya habari na mawasiliano pindi itakapo tumika italeta mabadiliko ya maendeleo katika mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.
“Iwapo technologia ya habari na mawasiliani sasa itatumika ipasavyo irahisisha ufanyaji utoaji wa maamuzi kwa mambo mbali mbali kwa wakati na kufikia malengo ya Nchi waliyojiwekea”Alisema Dkt Shein.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kupitia mkutano huo wa 50 kitu kikubwa walichojifunza kuwa Zanzibar ni sehemu ambayo watu wengi duniani watamani kuja kutembea kwa kujifunza historian na kutembelea vivitio vilivyopo.
“katika mkutano ambayo tumewahi uhudhuria ya chama cha jumuiya ya madola hakuna mkutano uliohudhu wa wajumbe wengi kama huu uliofanyika hapa Zanzibar hii inaonesha kuwa utalii wa Zanzibar upo juu na watu wengi wanahitaji kuja kwa lengo la kutembea na kujifunza vitu vilivyopo Zanzibar” alisema Job Ndugai.
Spika Ndugai alishauri serikali ya Mapinduzi y Zanzibar kuona kuwa kuna haja ya kuwekeza katika kujenga kubwa mbali mbali z mikutano kutokana na watu mbali mbali wanavutika kuja Zanzibar kufanya mukutano yao.
Mkutano huo unatarajiwa kujadili mambo mbali mbali kwa mustakabali wa mabunge ya Jumuiya hizo na kufungwa tarehe 5 septemba.
Ndugai aliongeza kusema kuwa katika mkutano huo wajumbe hao wa CPA wamekubaliana uwekezaji wa hoteli ya nyota tano mjini Dodoma na kwamba bado kikao kimoja kuhidhinisha jambo hilo
"Hoteli hii itakuwa ni mali ya CPA na hata hivyo tunawashukuru sana wenzetu kwa kutukubalia kufanyika kutokana na kuwa si jambo rahisi na endapo tukipata kibali hicho tutakwenda haraka sana kwenye ujenzi huo,"alisema
Alisema hivi karibuni katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano kutakuwepo na sheria ya e-goverment na kwamba katika sheria hiyo ndani yake kutakuwepo e-parliament na jambo hilo litakuwa sawa hakutakuwa na shaka lolote
Monday, September 2, 2019
Home
/
Top News
/
Dkt Shein awapa ushauri wabunge Jumuiya madola kutumia Technolojia ya Bunge Mtandao
Dkt Shein awapa ushauri wabunge Jumuiya madola kutumia Technolojia ya Bunge Mtandao
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment