Adbox

Friday, September 27, 2019

Baraza la Madiwani Halmashauri Tarime walia na madeni kuwalemea waomba serikali kuwalipia

Na Timothy Itembe Mara

Baraza la Halamshauri ya Tarime Mjini jana wamejadili kulemewa na Madeni kuanzia mwaka 2012 walioridhi kutoka halmashauri Mama  ya Tarime Vijijini wakati wa kugawana.

Kaimu mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Tarime kilichoketi jana katika ukumbi wa Shule ya sekondari Tarime,Daniel Komote kupitia Chama cha mapinduzi alisema kuwa halmashauri hiyo inadaiwa madeni  zaidi ya shilingi milioni 817 ya tangu mwaka 2012.

Komote alisema kuwa madeni hayo ni pamoja na madeni walioridhi kutoka halmashauri ya Tarime Vijijini wakati wanagawana halmashauri huku akibainisha kuwa madeni hayo yanachangiwa na madeni ya tenda ya chakula kwa shule za sekondari.

“Changamoto zinazoikumba halmashauri ya Tarime Mjini ni pamoja na  vyanzo tulivyo navyo kiduchu pamoja na baadhi ya vyanzo kama vle makusanyo ya kodi ya mazao kuondolewa makusanyo ya kodi ya Ardhi,makusanyo yavitambulisho vya wajasiliamali kuhamishiwa serikali kuu na kusababisha mapato kushuka pamoja na kubomolewa kwa vibanda vyasoko kuu ambalo linatajariwa  kujengwa kuwa la kisasa vilivyokuwa vinaingizia halmashauri yetu zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka”alisema Komote

Kwa upande wake diwani kata ya Kenyamanyori,Ganga  Mogendi aliomba halmashauri hiyo kuandika barua kwenda seikali kuu ili kuona namna ya kuwalipia na kuwapunguzia madeni.

Naye Mkuu wa soko la Rebu ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa sio msemaji alisema kuwa baadhi ya vyanzo makusanyo kuondolewa na vingine kuhamishiwa serikali kuu ndani ya soko wamebaki na makusanyo ya vibanda pamoja na ushuru wa magari ya ndizi mbichi za kusafirisha ambapo wafanyabiashara wengine ndani ya soko kama vile wa dagaa na mitumba  wanawaona tu wakifanya biashara bila kukusanya ushuru kutoka kwao.

Mkuu huyo alibainisha kuwa kabla ya vyanzo vya mapato havijaondolewa na vingine kuhamishiwa serikali kuu ndani ya Soko la Rebu tu walikuwa wanakusanya zaidi ya shilingi milioni moja kwa siku huku  kwa wili moja walikuwa wanakusanya shilingi milioni miamoja na zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Pedas Masungwa alisema kuwa madeni hayo watayalipa kutokana na fedha za makusanyo ya vyanzo vya ndani kadiri fedha itakapokuwa inapatikana.

No comments:

Post a Comment

Adbox