Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson atuhumu baadhi ya wabunge kushirikiano na Umoja wa Ulaya kuzuia Brexit.Boris Johnson, waziri mkuu mpya wa Uingereza awatuhumu baadhi ya wabunge kushirikiana na Umoja wa Ulaya kuzuia Brexit.
Johnson amejibu maswali katika ukurasa wake wa Facebook katika kipindi chake ambacho hurushwa kila wiki kinachoandaliwa bungeni, Boris amesema kuwa kuna ushirikian mbaya kati ya wale ambao wanadhani kuwa watazuia Brexit bungeni na rafiki zao Ulaya.
Kwa mujibu wa Boris Johnson, Umoja wa Ulaya hauna haja ya kufikia makubaliano na Uingereza kuhusu Brexit.
Hali ya vuta ni kuvuti inayoendelea kuhusu Brexit iwapo itazidi basi Uingereza italazimika kuondoka Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

No comments:
Post a Comment