Adbox

Tuesday, August 20, 2019

Tembeza mkong’oto kichwa kilie kama ngoma ya daku - RC Mwanri

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amelitaka Jeshi la Polisi kutowafumbia macho vibaka na na kuwatembezea mkong'oto kichwa kilie kama ngoma ya daku ili waache waseme "hii noma hapa tuondoke".

RC Mwanri ameyasema hayo aliposhiriki mapokezi ya Kamanda wa Polisi katika hafla iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa humo ambapo amewataka kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha kwa raia katika maeneo ambayo yanaviashiria vya uvunjifu wa amani.

“Majambazi hawawezi kuitisha mkutano kama huu na hawawezi kuandaa chakula kama hiki, wakatoa hotuba kama hizi tunazo zitoa hapa. Tutawashinda hawa watu kutokana na uhalali wa vita vyenyewe watu wawili hawawezi kutusumbua,” RC Mwanri.

"Tumeanzisha hilo jambo Mkoa mzima kibaka hawezi kutusumbua akitusumbua tembeza mkong'oto juu ya kichwa, kichwa kilie kama ngoma ya daku tatatataata! nyie cha kuchunga tu msije mkapitilisha akaondoka kwasababu mtakuwa mnavunja sheria, kichura weka kwenye maji, nyuma geuka, utasikia anasema hii noma hapa tuondoke."

No comments:

Post a Comment

Adbox