Adbox

Sunday, August 18, 2019

Samatta apiga hat trick, KRC Genk ikiibuka kidedea

Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, baada ya kuanza na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya nchini humo.kwa kupoteza michezo miwili jana imeanza kwa kishindo.

Genk iliyokuwa imepoteza michezo yake miwili kati ya minne niliyocheza, jana imeibuka na ushindi.mnono dhidi ya Waasaland Beveren kwa ushindi wa magoli 4-0.

Ushindi huo wa Genk ulichagizwa na hat trick ya Mbwana Samatta aliyefunga magoli matatu dakika ya 53, 66 na 86, hiyo baada ya Paintsil kufunga goli la Kwanza dakika ya 21, Samatta pia ametangazwa mchezaji bora wa mechi.

No comments:

Post a Comment

Adbox