Adbox

Wednesday, August 21, 2019

Rais Museveni na Kagame wakubaliana kumaliza mgogoro

Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wamesaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo jirani.


Walifikia makubaliano hayo katika mkutano wa pili huko Luanda mbele ya marais wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Angola na rais wa Congo Brazaville waliokuwa wapatanishi katika mgogoro huo.

Joto la kisiasa limekuwepo tangu mwanzoni mwa mwaka huu na liliathiri maisha ya watu katika Nyanja za kijamii na kiuchumi kwenye mataifa hayo jirani.

Maafisa nchini Rwanda wamekuwa wakiishutumu Uganda kwa kuwafunga na kuwatesa kinyume cha Sheria raia wake nchini Uganda, wakati Uganda nayo ikiishutumu Rwanda kutekeleza ujasusi katika ardhi yake.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kutilia mkazo kutatua mzozo wowote baina ya mataifa yao kwa njia za Amani, kwa mujibu wa Shirika la Habari nchini Angola.

No comments:

Post a Comment

Adbox