Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana, amezitaka Taasisi na watu binafsi wanaomiliki silaha, kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa ama kuibiwa na kutumika vibaya.
Kauli hiyo inakuja mara baada ya kijana mwenye umri wa miaka 19 Faisal Ibrahim, Mkazi wa Soko Kuu la Arusha, kujiua kwa kujipiga na risasi kichwani katika paji lake la uso kwa kutumia bunduki aina ya Rifle Wichester inayomilikiwa na Baba yake.
"Natoa wito kwa Makampuni, Taasisi na Watu binafsi wanaomiliki silaha, kutumia silaha hizo kwa umakini mkubwa na pia kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa au kuibiwa na kutumika vibaya" alisema.
Kijana huyo mwenye asili ya Kihindi alijipiga risasi hiyo majira ya saa 05:00 afajiri ya Agosti 18, huku chanzo cha tukio hilo kikielezwa kuwa ni msongo wa mawazo uliotokana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Monday, August 19, 2019
Polisi yawataka wanaomiliki silaha kihalali kuzitunza vizuri
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment