Adbox

Monday, August 12, 2019

Mikataba ya Geneva yatimiza miaka 70


Ni miaka 70 leo tangu kusainiwa kwa mikataba minne ya Geneva, iliyoweka msingi wa sheria ya kimataifa ya kulinda haki za binadamu. Lakini ingawa nchi 196 zimeitia saini mikataba hiyo, utekelezwaji wake unasuasua.Mikataba hiyo minne ya baada ya vita vikuu vya pili iliweka kanuni za kulinda haki za raia na wanajeshi katika mazingira ya vita. Ingawa nchi 196 ni wanachama wa mikataba hiyo, utekelezwaji wake wakati huu unakabiliwa na kitisho katika maeneo kadhaa ya mizozo.Kwa mujibu wa mikataba hiyo na itifaki kadhaa za nyongeza, raia na wanajeshi wanayo haki ya kutendewa ubinadamu katika mizozo ya kivita, na mashambulizi yoyote ya kijeshi yanaruhusiwa tu dhidi ya shabaha za kijeshi. Lakini, wakati mizozo ya kisasa ikijikita zaidi katika mazingira ya mjini, pande zinazohasimiana zimekuwa mara kwa mara zikiikiuka mikataba ya Geneva.

No comments:

Post a Comment

Adbox