Data za safari za baharini zinaonesha kwamba meli ya Iran iliyoko katikati ya mvutano kati ya Marekani na Iran imebadili mkondo kwa mara nyingine leo Ijumaa na inarudi tena Uturuki.
Ni mara ya tatu kwa meli hiyo ya Adrian Darya iliyokuwa ikifahamika pia kama Grace 1 kubadili kituo inachoelekea katika kipindi cha siku 10.
Iskenerun ni eneo lililoko kilomita 200 kutoka kaskazini mwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Baniyas nchini Syria, ambacho kinadhaniwa ndio kituo halisi inakoelekea meli hiyo ya Iran.
Marekani ambayo inasema meli hiyo inadhibitiwa na jeshi la kimapinduzi la Iran inaloliita ni kundi la kigaidi, imezionya nchi nyingine katika ukanda huo kutoisaidia meli hiyo.
Friday, August 30, 2019
Meli ya Iran inayoleta mvutano yabadili mkondo kurudi Uturuki
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment