Mchakato wa matumizi ya Sh. Bilioni 1.5 zilizotolewa wa Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa hospitali itakayozishirikisha kata za Buseresere na Katoro mkoani Geita na kuwanufaisha wakazi zaidi ya 100,000 umeanza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Said Kalidushi, alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Chato, Dk Medadi Kalemani, uliofanyika katika Kata ya Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wakiwemo viongozi wa chama na serkali wa kata za Katoro na Buseresere.
Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo Kalidushi alisema zilitolewa na Rais Magufuli mwezi uliopita alipokuwa mkoani Geita kufuatia kilio cha wakazi wa kata hizo zenye wakazi 100,000 ambao wamekuwa hawana hospitali yenye hadhi ya wilaya pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu.
"Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi..hatua hii ndiyo inayowafanya viongizi wa CCM kutembea vifua mbele kwani hiyo inatosha kuthibitisha kuwa ahadi zinatekelezeka mbali na mkakati wa ujenzi wa zahanati kwa kila kata kote nchini," aliisema Kalidushi.
Kwa upande wake, Dk Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati akielezea serikali inavyotekeleza Ilani ya CCM chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli alisema kumekuwepo na mabadiliko makubwa kuanzia ngazi za vijiji, kata na hata wilaya ikiwemo kuboreshwa kwa huduma za kijamii.
Aliwaomba Watanzania waendelee kumuamini Rais Magufuli kwani wao ni mashuhuda katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wake kumekuwa na mafanikio makubwa kama kurejea kwa nidhamu kwa watumishi wa umma, kujali maslahi yao na kuboreshwa kwa huduma za kijamii ambapo kila kunapokucha mambo makubwa yanafanyika.
Wednesday, August 14, 2019
Hospitali iliyopewa fedha na Rais Magufuli, Mchakato wa ujenzi waanza
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment