Waandamanaji mjini Hong Kong wameipuuza marufuku ya polisi ya kuwataka wasifanye maandamano na badala yake wameendelea kuandamana mabarabarani huku polisi nao wakitumia gesi ya kutoa machozi.Maandamano ya wanaharakati wanaotetea demokrasia katika jiji la Hong Kong, sasa yameingia katika mwezi wake wa tatu. Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika eneo la Victoria licha ya polisi kuupiga marufuku mkutano huo.Polisi pia waliwanyima waandamanaji hao idhini ya kufanya mkutano wa pili katika kitongoji cha Sham Shui Po. Licha ya katazo la polisi waandamanaji waliendelea na maandmano hata katika vitongoji vingine vya mji wa Hong Kong.China imelaani vikali ghasia zinazofanywa na waandamanaji ambao waliwatupia mabomu ya petroli maafisa wa polisi. China inmesema vitendo hivyo ni vya kigaidi.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hong Kong na Macao Yang Guang aliwaambia waandishi wa habari huko mjini Beijing kwamba waandamanaji wanatumia zana za hatari kuwashambulia maafisa wa polisi jambo ambalo linakiuka kabisa sheria na utaratibu wa kijamii wa Hong Kong. Lawrence Ma, mwanasheria na mwenyekiti wa Taasisi ya Sheria mjini Hong Kong, amesema zipo hatua za kisheria zinazoweza kuchukuliwa na serikali kwa mujibu wa katiba ili kudhibiti mambo.
Monday, August 12, 2019
Hong Kong: Safari zote za ndege za kuingia na kutoka zafutwa
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment