Adbox

Monday, August 5, 2019

Historia ya mataifa yaliyoendelea inatufundisha - Rais Magufuli


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa historia ya Mataifa yaliyoendelea inatufundisha kuwa hakuna njia ya mkato.

Rais Magufuli amesema kuwa kufikia uchumi mkubwa ni lazima tujikite kwenye uchumi wa viwanda.

"Historia ya mataifa yaliyoendelea inatufundisha hakuna njia ya mkato, kufikia uchumi mkubwa lazima, tujikite kwenye uchumi wa viwanda, viwanda ni muhimu katika kukuza uchumi, kuondoa umaskini na kuongeza ajira, viwanda ndivyo vimeziletea maendeleo makubwa nchi zilizoendelea," Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua maadhimsho ya Viwanda kwa nchi za SADC.

No comments:

Post a Comment

Adbox