Adbox

Saturday, August 10, 2019

Haya ndio Maagizo ya Rais Magufuli kwa Wizara kufuatia ajali ya Lori


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Wizara zote zinazohusika kushughulikia ajali iliyotokea Morogoro na ametaka Hospitali ya Mkoa wa huo kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhakikisha majeruhi wote wanapatiwa matibabu ili kuokoa maisha yao.

Rais Magufuli ameyasema hayo kupitia taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ambapo ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi ambapo Lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.

No comments:

Post a Comment

Adbox