Adbox

Friday, July 26, 2019

Waziri mkuu mpya wa Uingereza amteua kaka yake kuwa Waziri


Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amemteua kaka yake Jo Johnson kuwa waziri wa nchi.

Boris Johnson ambaye  Hapo jana alipokea madaraka ya uwaziri mkuu kutoka kwa mtangulizi wake ambaye alijiuzulu,Theresa May, amemteua kaka yake Jo Johnson katika baraza lake jipya la mawaziri kushika nafasi ya waziri wa nchi.

Jo Johnson amepewa majukumu mawili kama waziri wa nchi katika wizara ya uchumi, nishati na mikakati ya viwanda  pamoja na waziri anayeshughulikia vyuo vikuu na sayansi katika wizara ya elimu. Jo Johnson amepewa ruhusa ya kuhudhuria vikao vya mawaziri waandamizi.

 Waziri Johnson anatarajia kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31 iwe muafaka umepatikana au haujapatikana.

No comments:

Post a Comment

Adbox