Adbox

Thursday, July 11, 2019

Waandishi wa habari nchini waaswa kuzingatia Maadili

Waandishi wa Habari nchini wameaswa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo wakati wa kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa lengo la kuchochea ustawi wa wananchi wa nchi wanachama hasa fursa zilizopo.

Akizumzunza wakati akifunga mafunzo ya kundi la kwanza la waandishi wa habari watakaoripoti na kuandika habari za SADC leo mjini Morogoro Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Balozi Hebert   Mrango amesema kuwa, kila mwandishi analojukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu jumuiya hiyo na kwa wakati ili waweze kutumia fursa ya soko lililopo katika nchi 16 wanachama.

No comments:

Post a Comment

Adbox