Adbox

Tuesday, July 2, 2019

Tanzania yatolewa kinyonge AFCON, Hii ndio kauli ya Samatta








Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa
Stars baada ya kupoteza katika mchezo wao
wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Algeria kwa
 magoli 3-0, Mbwana Samatta ameongea na
waandishi na kueleza kupokea kwa masikitiko
matokeo hayo lakini akieleza hiyo ni kama fursa
 kwao ya kujua michuano hiyo na kupata uzoefu.
“Ni mashindano makubwa namshukuru 
Mungu nimeweza kucheza mechi zote nipo
 salama lakini nadhani nahitajika zaidi kufanya 
bidii zaidi ya nilizokuwa nazifanya kwa sababu
 nimeona kuna ugumu wake kucheza na timu
 kama hizi hapa ambazo zimepiga hatua sana
 lakini kama timu tuna safari naona”>>>Samatta
“Nashukuru Mungu tumepata nafasi ya kuwa 
katika mashindano haya ni kitu ambacho kiukweli 
kimetufundisha kwa kiasi kikubwa safari yetu bado
ipo tunahitaji kufanya bidiii, bado kuna safari kuna
mlima mkubwa inabidi tuushinde kila eneo, nadhani 
vitu ni vingi tu maandalizi wachezaji nafikiri wanahitaji 
kwenda kucheza proffesional wengi sana ili kuweza 
kuendana na mashindano kama haya”>>>Samatta
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa matokeo
hayo imeondolewa rasmi kwa kuwa nafasi ya mwisho
katika Kundi C ambalo lina timu za Algeria anayeongoza
kwa kuwa na point 9, wakifuatiwa na Senegal wenye
point 6 na Kenya nafasi ya tatu kwa kuwa na point tatu
walizozivuna dhidi ya Tanzania.
Aliyeiua Taifa Stars (Olunga) kataja walipokwama Tanzania

No comments:

Post a Comment

Adbox