Mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bi Sada Malunde amewataka wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani humo kuchimba madini kulingana na leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini hayo kama zilivyotolewa na serikali kupitia tume ya madini hapa nchini.
Bi, Sada amesema hayo wakati akizindua soko la madini ya dhahabu wilayani biharamulo mkoani kagera kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Elisha Marco Gaguti ambapo amesema kuwa uzalishaji wa dhahabu wilayani humo ni mdogo ukilinganisha na leseni zilizopo na zinazofanya kazi. Ambapo amewataka wamiliki wote wa leseni za uchimbaji madini ya dhaabu kuanza kuzitumia mara moja.
Kwa upande wake afisa madini mkoa Kagera bw, Lukasi Mulekwa amesema kuwa hii ni fursa kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani humo kuongeza kasi ya uchimbaji ambapo kwa sasa wanazalisha gram 200 ya madini ya dhahabu kwa mwezi sawa na gram 2000 kwa mwaka ambapo ukilinganisha na leseni walizotoa 244 ni leseni tano tu zinazofanya kazi.



No comments:
Post a Comment