Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa saba tajiri zaidi duniani - G7 wanakutana mjini Chantilly kaskazini mwa Paris, Ufaransa kwa ajili ya mkutano wa siku mbili unaolenga kutafuta msimamo wa pamoja wa suala tata la kodi kwa makampuni makubwa ya teknolojia lakini pia wataangazia hatari ya sarafu mpya za kidijitali.
Mwenyeji wa mkutano huo, waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire ameungana na wenzake hii leo kwenye mkutano huo unaoyakutanisha mataifa ya Ujerumani, Uingereza, Italia, Canada, Japan na Marekani.
Mawaziri hao wanakutana katika wakati ambapo kuna sintofahamu kuhusiana na kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia pamoja na sera za biashara za rais wa Marekani Donald Trump za Marekani Kwanza, zilizosababisha vita vya kibiashara na China, na hali ya wasiwasi na Ulaya.
Mkutano huu unasafisha njia ya mkutano wa kilele utakaowakutanisha wakuu wa mataifa na serikali za Kundi la G7, unaotarajiwa kufanyika kati ya Agosti 24 na 26 katika mji wa Basques, nchini Ufaransa.
Wednesday, July 17, 2019
Mawaziri wa fedha wa G7 wakutana Ufaransa
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Habari za kimataifa
Tags:
Habari za kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment