Kocha wa Man United, Ole Gunnar Soslkjaer amethibitisha kuwa Pogba haendi popote. Ole amewaambia waandishi wa habari kuwa unapokuwa na mchezaji kama Pogba kwenye timu yako, lazima uijenge timu kumzunguka yeye.
Amedokeza kuwa ni lazima Pogba alindwe kutokana na kipaji alicho nacho, na njia pekee ya kumlinda Pogba ni kuhakikisha wote kwa pamoja wanapambana kupata mataji.
"Kucheza United pekee sio kitu kama hunyakui mataji. Hii inaleta hofu ndio maana hata wachezaji wenyewe wanaweza kutamani kuondoka" alisema Ole Gunnar
Alipoulizwa pia kuhusu usajili, amekiri klabu yake kuhitaji wachezaji wawili au hata watatu. Lakini ametoa tahadhari kuwa, kuja kwa wachezaji wapya itabidi kuambatane na baadhi ya wachezaji kuondoka.
Wednesday, July 17, 2019
Man United wasema Pogba haendi popote
Tags
# Michezo
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Michezo
Tags:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment