Boris Johnson amechukua rasmi nafasi ya kuwa waziri Mkuu nchini Uingereza baada ya Theresa May kujiuzulu.
Meya huyo wa zamani wa jiji la London aliye na miaka 55 amechukua rasmi Jumatano nafasi ya Waziri Mkuu punde tu baada ya Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza kumuomba kuunda serikali.
Waziri Mkuu huyo mpya ana miezi mitatu tu ya kutengeneza pale Bi May aliposhindwa na kufanikisha ahadi zake za kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31.
Boris Johnson tayari ameshamteua Dominic Cummings kama mshauri mkuu wake.
Alipokuwa anafungasha virago na kuondoka katika ofisi yake ya Downing Street, Bi Theresa May alisema anafurahi kuwa mrithi wake Boris Jonhson ana nia ya kutimiza kile raia wa Uingereza walichokitaka, baada ya kupiga kura ya maoni mwaka 2016 kuondoka katika Umoja wa Ulaya.
Theresa May alisema bado ataendelea na majukumu yake mengine serikalini kama mbunge wa kawaida.
May alitingisha kichwa baada ya kuulizwa na kiongozi wa chama cha upinzani Jeremy Corbyn kama atajiunga nao ili kuzuwiya mipango ya Brexit ya Boris Johnson aliyeahidi kuindoa nchi hiyo katika Umoja wa Ulaya ifikapo Oktoba 31 kwa makubaliano au bila makubaliano.

Viongozi kadhaa wajiuzulu kabla ya Boris Johnson kuchukua ofisi ya Waziri Mkuu
Wakati huo huo, Waziri wa Fedha wa Uingereza, Philip Hammond anayeupinga mpango wa Brexit amejiuzulu muda mchache kabla ya Boris Johnson kuwa waziri Mkuu wa Uingereza.

No comments:
Post a Comment