Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa tayari upelelezi wa wafuasi 27 wa CHADEMA, umekwishakamilika na kesho watalipeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zingine.
"Walikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wamekusanyika kwenye geti la kuingilia Gerezani, na kutaka kulazimisha kuingia kwa nguvu, getini pale kuna ulinzi, walitumia nguvu, ambapo hata Askari aliyekuwa lindo alichaniwa sare yake, kwahiyo wao walitaka kwenda kumtoa Mwenyekiti wa chama hicho bila kukamilisha taratibu" amesema Kamanda Mambosasa.


No comments:
Post a Comment