Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema wanawashikilia wanawake watatu kwa tuhuma za na kujihusisha na kusafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi, wakitokea Nje ya nchi na kuyaingiza nchini.
Kamanda Malimi, amesema wanawake hao walikamatiwa katika eneo la Kyakailabwa lililopo katika Manispaa ya Bukoba, wakiwa katika magari yaliyokuwa yakifuatiliwa na Polisi, baada ya kuyatilia shaka, ambapo walikuwa wamejifunga mabunda zaidi ya 50 kwenye miili yao.
Kamanda Malimi amewtaja wanawake hao ni Vivian Charles (29) mkazi wa Kagondo, Anchila Wilson miaka 29, mkazi wa Nyanga na Slyvia John miaka 32 mkazi wa Kyakailabwa, wote katika Manispaa hiyo.
Kamanda Malimi amesema Jeshi hilo linatarajiwa kuwafikisha Mahakamani wanawake hao.
Sunday, November 24, 2019
Wanawake watatu mbaroni kwa kusafirisha madawa ya kulevya
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment