Adbox

Saturday, August 17, 2019

Sudan kusherehekea makubaliano ya kihistoria

Sudan itasheherekea hii leo makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa kati ya majenerali wa kijeshi na viongozi wa waandamanaji, juu ya kuundwa kwa serikali ya kiraia, ambayo wengi wanatumai italeta mafanikio.

Katika sherehe hiyo itakayofanyika katika ukumbi mmoja mjini Khartoum, wanachama wa baraza la mpito la kijeshi na viongozi wa waandamanaji watatia saini nyaraka katika hafla hiyo.

Mpango huo uliofikiwa Agosti 4 unaashiria kumalizika kwa mgogoro wa kisiasa wa takriban miezi minane. Kabla ya hapo raia wengi wa Sudan waliandamana kupinga utawala wa Omar al Bashir ambaye hatimaye aliondolewa madarakani mwezi Aprili baada ya kuiongoza Sudan kwa miaka 30.

Muundo wa baraza kuu la mpito lenye wingi wa wajumbe wa kiraia litatangazwa rasmi hapo kesho Jumapili.

No comments:

Post a Comment

Adbox