Adbox

Monday, July 15, 2019

Waziri Mkuu akabidhi Tsh. Milioni 2.5 kwa Mjasiriamali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Bw. Leonard Nkamba wa kijiji cha Kambanga wilayani Kasulu msaada wa sh. milioni 2.5 ili zimwezesha kununua vitendea kazi vya kisasa vya kumsadia kufanya kazi yake ya kuchonga vyombo mbalimbali vya mezani kwa kutumia miti. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Kigoma Julai 24, 2019.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Waziri Mkuu, mjasiliamali huyo amesema anaushukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambao uliona kazi zake na kumuagiza atengeneze seti za vyombo kwa ajili ya zawadi za kumpelekea Rais Dkt. John Magufuli.

“Uongozi wa UWT mkoa wa Kigoma Taifa ulivutiwa na kazi zangu na kuniagiza nitengeneze chupa ya chai, vikombe na hot pot kwa ajili ya kumpa zawadi Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu ndipo Waziri Mkuu jana aliona kazi zangu na akavutiwa na bidhaa ninazotengeneza ndipo akaniuliza kama kuna changamoto zinazonikabili nikamwabia nahitaji mashine moja yenye thamani ya sh. milioni mbili na nusu akasema umepata na leo sijaamini alivyoniita na kunikabidhi. Namshukuru sana.” amesema.

Nkamata ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wengine hususani vijana waache kulalamikia suala la ukosefu wa ajira na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wataziuza na kujipatia kipato

No comments:

Post a Comment

Adbox