Adbox

Tuesday, October 22, 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Afya ahitimisha ziara yake mkoani Mara

Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula amehitimisha ziara yake mkoani Mara kwa kutembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Kwanga) na kuona maendeleo ya ujenzi ulioanza toka mwaka 1975 lakini ukawa unasuasua kutokana na sababu mbalimbali.

Dkt. Chaula amemtaka mkandarasi mkuu Shirika la nyumba nchini (NHC) kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Agosti mwaka 2020 baada ya kupewa fedha zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, na ametaka huduma zianze kutolewa mapema kwani Hospitali hiyo itakua ni mkombozi kwa wananchi wa Musoma na maeneo jirani wanaopata rufaa za kwenda Bugando.

Baada ya hapo Dkt. Chaula ametembelea Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Musoma na kuona hali halisi ya utoaji wa huduma za afya Hospitalini hapo kisha kuongea na watumishi.

Aidha, Dkt. Chaula amehitimisha ziara yake mkoani Mara kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Butiama na kuridhishwa na majengo mapya ya huduma za mama na mtoto na kisha kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa na kuweka shada kwenye kaburi lake.

No comments:

Post a Comment

Adbox